Timu ya Young Africans imerudi kileleni
kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kupata ushindi wa
bao 2-0 dhidi ya wajelajela wa tanzania,Tanzania Prison toka jijini
mbeya mchezo uliochezwa pale uwanja wa taifa.
Yanga wanashikilia usukani ijapokuwa
wanafanana idadi ya pointi na watani wao wa jadi Simba SC,lakini
wanawaacha mbali kwa idadi kubwa ya magoli kwa sasa.
Yanga walipata bao lao la kwanza toka
kwa Amis Tamwe dk ya 71 na goli la pili lilifungwa na Obrey chilwa
mnamo dk 75 ya mchezo na kuifanya timu hiyo kutoka kifua mbele kwa
goli hizo 2-0 mpaka kipemga cha mwisho kilipopulizwa.
No comments:
Post a Comment