Timu ya Serengeti Boys imewasili jijini
Dar es Salaam ikitokea Gabon ilipokua ikishiriki michuano ya AFCON
U17 ambapo walitolewa Niger kwa bao 1-0,kwenye mchezo wa mwisho wa
kundi B.
Dkt. Harrison Mwakyembe ,Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo aliungana na watanzania na
wapenda michezo waliojitokeza uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl.
J.K Nyerere. Kuwapokea vijana hawa wa timu ya taifa ya vijana.
“Karibuni vijana wangu,
mmeliwakilisha taifa vizuri ,hii inaonesha ni jinsi gani tunakuwa
washindani dhidi ya mataifa mengine kwa kadri siku zinavyosonga
mbele,ni wakati muafaka wa kufanya maandalizi ya kutosha ili wakati
ujao kombe lije nyumbani”.
No comments:
Post a Comment