Timu ya soka yawana jangwani " Yanga" ya Dar es salaam imefikisha pointi 68,baada ya kuichapa timu ya
Toto Africans kwa goli 1-0,na kuwafanya warudi kileleni mwa ligi kuu ya soka Tanzania bara.
Goli pekee la
Yanga liliwekwa wavuni na Amis Tambwe kunako dakika ya 81 ya mchezo
na kuwafanya watoke kifua mbele na kujinyakulia pointi tatu muhimu
katika mchezo huo.
Timu hii ya wana
jangwani inalitafuta kombe hili la ubingwa wa ligi kuu,kwa udi na
uvumba ili kuweza kukamilisha misimu mitatu mfululizo katika
kulichukua ambapo misimu miwili ya nyuma walinyakua kombe hilo.
Mpaka sasa wapo
kwenye nafasi nzuri ya kulichukua kombe hilo linalonyemelewa kwa
ukaribu na wapinzani wao timu ya wekundu wa msimbazi “Simba SC” .
No comments:
Post a Comment