Serengeti
Boys imejitupa uwanjani kwenye mchezo wake wa pili dhidi ya Angola
kwenye michuano ya AFCON U17 .
Mchezo
ambao kwa Serengeti Boys waliuchukulia kwa umuhimu wa hali ya juu
kwa kutafuta matokeo ya ushindi ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya
kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo.
Ambapo
kwenye mchezo huo serengeti boys wamefanikiwa kuikata kiu yao ya
kuusaka ushindi kwa kutoka kifua mbele kwa kuwafunga Angola mabao 2-1,kwenye
mchezo uliochezwa pale uwanja wa “Stade L'Amitie”.
huku
magoli hayo ya serengeti boys yakifungwa na Naftal dakika ya 6,wakati
Suleiman akitikisa wavu dakika 69 ya mchezo.wakati goli pekee la
angola likifungwa na Pedro dakika ya 14 hivyo mpaka mchezo
unamalizika vijana wakitanzania walijawa na matumaini ya kuvuka hatua
ya nusu fainali ya michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment