Timu
ya taifa ya Mali walio mabingwa watetezi wa michuano ya AFCON
U-17,imekuja na matokeo mazuri baada ya kukutana na Niger kwenye
mchezo uliochezwa pale nchini Gabon kwenye michuano inayoendelea
ndani ya uwanja wa Stade l'Amitie
Ambapo
mali wamefanikiwa kuibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 2-1,magoli
yaliyofungwa na wachezaji Hadji Drame'7 Mohamed Camara'45,huku goli la
Niger liliwekwa wavuni na Habibou Sofiane'36.
Kwa
sasa mabingwa hawa watetezi timu ya Mali U17,wapo sawa na timu ya
Taifa ya Tanzania “Serengeti boys” kutoka Tanzania kwa kila timu
kujinyakulia pointi nne mkononi.
Ijapokuwa
Serengeti Boys hata kama ikipata sare kwenye mchezo wao unaofuatia
wanaweza kuvuka hatua nyingine lakini wanapaswa kuutazama ushindi kwa
macho mawili ili kujiwekea rekodi nzuri kwenye michuano na uhakika
mkubwa wa kusonga mbele.
No comments:
Post a Comment