Rapa Roma Mkatoliki aliyewahi
kupata matatizo ya kutekwa akiwa na wenzake waliowahi kutekwa na watu
wasiojulikana na kushikiliwa kwa siku kadhaa amesema bado hawajakaa
sawa tangu tukio hilo lililotokea japokuwa analazimika kurudi kazini
ili kujipatia kipato.
Ameongea machache alipAkiwa kwenye kipindi cha XXL
ya Clouds fm leo, Roma amesema waliathiriwa sana na tukio hilo,ambapo
vifaa vya studio ya Tongwe Records vilichukuliwa na kazi
zao nyingi kupotea.
"Hatuko poa sana, lakini lazima tutoke tufanye kazi. Tulipata madhara makubwa kwenye Studio yetu Tongwe Records, baada ya kuchukuliwa vifaa vyetu. Nimepoteza album nzima na muziki ni hisia. Hivyo mpaka nitulie ndio nitaandika ngoma nyingine. Kwa sasa naomba msupport zilizopo. Mdogo wangu Moni Centrozone ana ngoma kali ametoa, inaitwa Tunaishi nao." alisisitiza Roma.
No comments:
Post a Comment