Timu
ya Taifa ya vijana yaTanzania chini ya umri wa miaka 17 Serengeti
Boys kesho Mei 15 2017 itacheza mchezo wake wa kwanza wa Kundi B wa
michuano ya AFCON U-17 dhidi ya timu ya taifa ya Mali ambao ndio
Mabingwa watetezi wa Kombe hilo.
Kocha wa
serengeti boys “Bakari shime“amesema wachezaji wake wako vizuri
kimwili na kiakili na wamekuwa wakionesha morali ya kutaka kuwa
machampioni wa mashindano hayo,anatambua na kuheshimu timu ya mali
kwa kuwa mabingwa watetezi lakini vijana na benchi la ufundi
wamejizatiti kwa mchezo huo.
Aidha ameishukuru TFF na watanzania kwa ujumla kwa kuendelea kuonesha mchango na nguvu kubwa katika kufanikisha timu kufika huko kwa wakati na kukiwezesha kikosi kuwa na muda mzuri wa maandalizi.
No comments:
Post a Comment