Kampuni Toyotaya kuunda magari toka
Japan, imetangaza kuunga mkono kundi la wahandisi lililo katika
jitihada za kuunda gari linaloruka na kupaa.
Toyota imesema kuwa inatoa kiasi
cha dola 300,000 kwa kundi la wahandisi ambalo huendesha shughuli zake nje ya
mji wa Toyota kati kati mwa Japan.katika kufanikisha mpango huo kundi
hilo limeendelea kupata sapoti kutoka kwa wadau mbalimbali
watakaowezesha kukamilika kwa uundwaji wa gari hilo.
Kutokana na teknolojia
wanayoendelea kuitumia inayoendana na mfumo wandege katika kulifanya
gari lililo na umbo dogo kuweza kuruka na kuja kutumika katika
maonesho mbali mbali makubwa duniani.
No comments:
Post a Comment