Kwenye vikao vinavyoendelea bungeni
Mbunge wa Mtama Mh Nape Nnauye ataka kujua juuya tatizo la
mawasiliano jimboni kwake,ambapo ameuliza serikali iweke wazi ni lini
tatizo la minara ya mawasiliano itakamilika ili kuunganisha
mawasiliano kwenye eneo kubwa la jimbo lake ambalo halijafikiwa na
hudoma hiyo.
Ambapo amesema kati ya tarafa tano,tatu
hazina mawasiliano ya simu.Aidha serikali kupitia waziri husika
ilikuja na jibu “kuwa haikubaliki kuwa tarafa hizo tatu hazina
mawasiliano hivyo serikali inafuatilia kwa wale walioanza kuweka
minara ya mawasiliano ya simu,na kuweza kuweka msukumo ili
kuwapelekea wananchi huduma hiyo”.
Pia serikali inatambua maeneo mengi yaliyo pembezoni mwa nchi hayajafikiwa na huduma ya kuwaunganisha kimawasiliano kutokana na jiografia ya maeneo,lakini yanaendelea kuangaliwa ili kuleta muunganiko wa kimawasiliano utakaowawezesha wananchi waweze kuunganishwa na huduma za kimawasiliano kama sehemu nyingine ambazo zimeshaunganishwa.
No comments:
Post a Comment