Rais
mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, ameapishwa leo ikiwa ni wiki moja
imepita tangu alipopata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu wa
Urais nchini humo.
Bwana
Macron ambaye ni Rais mdogo zaidi kiumri kuwahi kutokea nchini
Ufaransa, ameahidi kufufua uchumi wa Ufaransa na kuleta mabadiliko
kwenye mfumo wa siasa uliokuwa ukitumiwa hapo kabla.amesema anaamini
atayaweza hayo yote kwa kupitia chama chake kipya cha The Republic on
the Move.
Wachambuzi
wa Masuala ya Kisiasa wanasema Rais Macron atashindwa kuleta
mabadiliko aliyoyaahidi kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake Francois
Hollande, ambaye aliahidi mabadiliko, lakini mpaka anaondoka amekuwa
Rais asiye na umaarufu katika historia ya Ufaransa.
No comments:
Post a Comment