Baada ya Korea Kaskazini, kufanyia
majaribio ya kombora la masafa marefu, lililorushwa karibu na mji wa Kusong kaskazini magharibi mwa nchi hiyo na kuanguka katika bahari ya
Japan,kwenye mpango wake wa zana zake za nyuklia,Marekani
imesisitiza kuwekwa vikwazo zaidi kwa taifa hilo.
Hata hivyo mataifa kadhaa yamekuwa
yakipingana na mpango huo wa korea Kasskazini,ikiwemo nchi ya Korea
kusini kupitia Rais wao mpya Moon Jae-in,ambaye amelaani kitendo
hicho cha majirani zao cha kufanya majaribio zaidi ya zana zake za
mafasa marefu.
Hii imekuja baada ya Jaribio la
awali kushindwa kukamilika,Lakini imeendelea kuonekana kuwa Korea
Kaskazini imekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa pamoja na vikwazo
kadhaa ambavyo vimeonekana kuwa vitazaa matunda katika kusitishwa kwa
mpango huo wa zana hizo.
No comments:
Post a Comment