Lowassa aongelea mambo kadhaa ikiwemo suala la vyeti feki,aiomba
serikali kuwaonea huruma watumishi hao kwa kuwatazama kwa jicho la
huruma kwakuwa wengi wao wametumika kwa muda mrefu na wana familia
ambazo zinawatazama.amesema kuwa haungi mkono kwa walichokifanya
lakini itafaa wakifikiriwa japo kidogo.
Amedai kuwa ingependeza sana kama Rais John Pombe Magufuli
angehudhuria kwenye kuagwa kwa watoto na walimu wao walipokuwa
wakiagwa pale Arusha na sio kupeleka mwakilishi,ambaye ni makamu wa
rais mama Samia Suluhu Hassani.
Ameongelea pia suala la ukuaji katika matumizi ya mitandao ya
kijamii,ambapo amesema kuwa wakati mwingine inasaidia kufikisha
ujumbe kwa watu wengi zaidi kwa muda mchache.
No comments:
Post a Comment