• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Sunday, 21 May 2017

    Serengeti Boys na huzuni ya kupokonywa tonge mdomoni,huko Gabon AFCON u17.

    Macho na masikio ya watanzania na wana afrika mashariki wengi yalitupiwa kule nchini Gabon ambapo yale mashindano ya AFCON U17 yameendelea kwa timu ya Serengeti Boys kucheza na Niger kwenye mchezo wa kundi B.

    Kwenye mchezo huo,vijana wa Serengeti Boys walionekana kuwa na morali ya mchezo na kuonesha kuhamasishana sana,hata kabla ya mchezo kuanza, lakini walijikuta wakikabiliana na wakati mgumu toka kwa wapinzani wao Niger U17.

    Mchezaji Marou wa Niger” ndiye aliyeucheza mpira kwenye dakika ya 42,mpira ambao ndio ulioleta madhara kwenye lango la Serengeti Boys,na hata kuwafanya wayaage mashindano hayo baada ya kupoteza mchezo huo kwa goli 1-0.wakati huo mabingwa watetezi Mali U17 ikipeta kwa kuwa pointi 7 kibindoni,wakifuatiwa na Niger ambao wanalingana pointi na Serengeti Boys lakini wakiwa na goli la faida lililowavusha.

    No comments:

    Post a Comment