• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Sunday, 21 May 2017

    Diamond Platnumz na Label ya WCB,wanataka kumtambulisha msanii wao mpya.

    Diamond Platnumz na wasanii wote wa WCB na uongozi wao wote,kesho wanatarajia kumtambulisha msanii mwingine ndani ya label hiyo kubwa kwa sasa hapa bongo na africa mashariki.

    Ambayo imeonekana kuwawezesha vijana tofauti kufikia malengo yao kwa kupitia vipaji walivyonavyo,wcb ilianza na msanii Harmonize,rayvanny,Rich Mavoko,Queen Darleen,na sasa mambo yameiva zaidi ataletwa kijana mwingine toka mtaani.

    Tumepata dokezo hili toka kwa Diamond Platnumz”Simba' mwenyewe kupitia ukurasa wake wa instagram kwa maneno haya:......

    Panapo majaaliwa siku ya jumatatu kesho, ntakuwepo kwenye LEO TENA ya Clouds fm na familia nzima ya @Wcb_wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu Mwingine Mpya toka Mtaani, ndani ya @Wcb_Wasafi..... Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umasikini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini... na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake....Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha...Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji...na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo...... USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi...Shukran”- ameandika Diamondplatnumz 

    No comments:

    Post a Comment