Yule Rapa wa kike anayejiamini na kujua nini anafanya,namzungumzia
mwanadada “Chemical” ni nembo kwa wadada wotewanaojiamini na
wenye kuweza kukabiliana na changamoto kwenye safari yake ya muziki
na hata maisha ya kawaida.
Siku zote ameonekana kuwa muwazi kwenye maisha yake,na kusimama
kwenye kile anachokiamini ameonekana ni mtu anayeendelea kusimamia
misimamo na jambo lake kukua.baada ya kupitiwa na vuguvugu la
kumwagiwa hadharani hisia za mapenzi mazito toka kwa mwanamuziki
mwenzake “Stereo” ambapo naye aliweka bayana hisia zake na kuweza
kuupa nafasi muziki wake kwanza.
Kwa sasa kaja na ngoma kali nyingine inayokwenda kwa jina la “Marry Marry” uliorekodiwa ndani ya studio za kazi kwanza chini ya mtayarishaji MaxMizer “ambayo imeendelea kudhihirisha uwezo wake wazi wazi,nafikiri hii inaweza kuonesha ni jinsi gani amedhamiria kuonesha ulimwengu kuwa ukisimama kwa kile unachokiamini utafika unapopataka.
No comments:
Post a Comment