Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Aprili 2017, ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi, Parokia ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio ndio nguzo na chachu ya Maendeleo.
Aidha Rais Magufuli(JPM) aliwaambia haya waumini na Taifa kwa ujumla ikiwa ni ujumbe wake wa siku ya siku ya jumapili kupitia ibada hizo...
“Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu
Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa
wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili
kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu” alisema
Rais Magufuli
“Nafikiri mnaweza mkaona sura yangu, kuna wanaonitafsiri kama
mtu katili, wa ajabu,lakini siko hivyo, mimi ni mpole, mnyenyekevu,
mwenye upendo mkubwa, ninayeogopa dhambi na mwenye hofu ya Mungu
lakini, ukweli mimi ni mkali kwa maovu” alisisitiza Rais Magufuli.
No comments:
Post a Comment