Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania
chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imepata ushindi wa tatu
mfululizo ikiwa ugenini amabpo imeweka kambi maalum kwa ajili ya
maandalizi kujiandaa na mashindano ya AFCON kwa vijana chini ya miaka
17 itakayoanza mwezi Mei 14, 2017.
Serengeti Boys wameifunga timu ya
taifa ya vijana ya Cameroon kwa goli 1-0 lililofungwa na Ally Ng’anzi
kipindi cha kwanza katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ambao
unakuwa ni mchezo wa tatu Serengeti kushinda mfululizo.
Baada ya kumaliza kambi nchini
Cameroon itaondoka na kuelekea moja kwa moja Gabon ambako zitafanyika
fainali za michuano hiyo ya vijana itakayoshirikisha mataifa nane
No comments:
Post a Comment