Saa chache tu baada ya kumalizika kwa pambano la ndondi lililoziteka hisia za wapenzi wengi wa ndondi duniani ambapo bondia wa Uingereza Anthony Joshua ameshinda kwa KO katika round ya 11 dhidi ya raia wa Ukraine Wladmir Klitschko, sasa ametaka pambano dhidi ya bingwa wa zamani wa uzito wa juu Mwingereza mwenzake Tyson Fury.
Katika
interview baada ya pambano dhidi ya Wladimir Klitschko lililopigwa
katika Uwanja wa Wembley jijini London na kushinda kwa KO raundi ya
11, Joshua alimuomba Fury ambaye ni Mwingereza mwenzie
wazichape:“Fury, Tyson Fury, uko wapi baby? Ni hiki unachotaka
kuona? Nafurahia kupigana, napenda kupigana.
"Tyson
Fury", najua ulikuwa unaongea sana na unataka kurudi na kushindana –
nataka kuwapa watu 90,000 nafasi ya kuangalia usiku mwingine wa
boxing. Nataka kupigana na kila mtu, nafurahia hii sasa.”Anthony
Joshua.
Naye
bondia bingwa wa zamani katika ngumi hizo za uzito wa juu Tyson Fury
alimjibu Anthony Joshua kwa kupitia akaunti yake ya mtandao wa
twitter baada ya kusikia tambo hizo akisema amekubali kupambana
ambapo aliandika:“Anthony Joshua umekubaliwa. Tutaupa ulimwengu
pambano kubwa katika miaka 500. Nitacheza na wewe.” Tyson Fury.
No comments:
Post a Comment