Jumapili
ya leo ya tarehe 30 Aprili 2017 ni siku ya historia mpya kwa timu
changa katika ligi kuu hapa Tanzania Bara maarufu kama VPL kwa klabu
ya soka ya Mbao FC ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza katika ligi
hiyo kutoka jijini Mwanza imefuzu kucheza fainali ya FA Cup au
maarufu kama Azam Sports Federation Cup kwa kuwang'oa mabingwa
watetezi wa kombe hilo Yanga SC ya Dar es Salaam.
Wakiwa
wamepanda daraja kutoka ligi kuu Tanzania bara kwa mara ya kwanza,
wameweza kufuzu kucheza fainali ya kwanza katika historia yao kwa
kuifunga Yanga kwa goli 1-0 katika mchezo wa nusu fainali uliochezwa
kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.Goli pekee la ushindi wa
Mbao FC lilitokana na kujifunga kwa mlinzi wa kati wa Yanga Vicent
Andrew katika dakika ya 27 ya kipindi cha kwanza wakati akiwa katika
harakati za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na mchezaji Pius Buswita
wa Mbao FC.
Matokeo
hayo yanaivua Yanga ubingwa wa FA Cup (Azam Sports Federation Cup)
ubingwa ambao waliutwaa mwaka uliopita kwa kuifunga Azam kwenye
mchezo wa fainali.Hivyo Mbao FC watakutana na Simba SC kwenye mchezo
wa fainali, mechi ambayo Simba ndio wanatarajiwa kuwa wenyeji kwa
sababu ndio walikuwa wa kwanza kufuzu kucheza fainali baada ya
kuifunga Azam FC kwenye mchezo wa nusu fainali uliochezwa hapo jana
kwenye uwanja wa taifa
No comments:
Post a Comment