Kiongozi
wa kanisa Katoliki Papa Francis anapendekeza ufanyike mjadala wa
kimataifa wa kuleta suluhu ya mvutano unaozidi kutokota kati ya
Marekani na Korea kaskazini.Papa Francis amesisitiza kuwa migogoro wowote ni vyema ukiisha kwa njia ya meza ya mazungumzo.
Amesema
kwamba umoja wa mataifa unatakiwa kufanya kazi ya ziada kwenye
hili,kwani hapo nyuma kidogo manoari za kimarekani zilitia nanga huko
rasi ya korea.na ni kwa mara kadhaa Rais wa Marekani Donald Trump ameonesha kuishutumu Korea Kaskazini kwenye mpango wake wa nyuklia.
baraza
la ulinzi la Umoja wa Mataifa lilikaa na kujadili mpango wa nyuklia
wa Korea Kaskazini lakini baadae kidogo lilifanyika Jaribo la kombora
la Korea Kaskazini ambalo halikufanikiwa.
No comments:
Post a Comment