Rais wa Marekani Donald Trump amesema atahakikisha anazisaidia
Israel na Palestina kupata amani,aidha amemshukuru Rais Mahmoud
Abbas,kiongozi wa Palestina kwa kuonesha jitihada zinazohitajika
kupiga vita ugaidi
Donald Trump ambaye anamalizia ziara yake mashariki ya
kati leo,anasema anajua kuwa makubaliano kati ya pande hizi mbili
yatakuwa na ugumu wa aina yake lakini ana imani yataenda kufanikiwa na
anatambua kuwa pande hizi mbili zina takribani miaka mitatu
hazijazungumza kwa ukaribu,lakini kwa uwepo wake mambo yatakaa sawa.
Trump alisema atahakikisha anaimarisha pia uhusiano usiovunjika
kati ya Marekani na Israel,Amekuwa akieleza kuwa eneo lililotawaliwa
na ghasia nyingi na vurugu ambapo wafadhiri wake wako wazi wazi ni
hatari.
No comments:
Post a Comment