Kampuni ya Kubashiri ya SportPesa
imeingia imeingia mkataba na timu ya Singida United ili kuidhamini
timu hiyo,wawakilishi wa singida united waliokwenda kuweka sawa mambo
mazima ya kukamilisha zoezi hilo,mmoja akiwa ni Katibu Mwenezi wa
Singida United “Festo Sanga”na CEO wa SportPesa “Pavel
Slavkov”.ambaye ametanabaisha kwamba Mkataba wa udhamini wa
SportPesa na Klabu ya Singida United utakuwa ni wa mwaka mmoja na
wenye thamani ya Shilingi milioni 250 za kitanzania.
Baada ya mkataba huu Singida United
ya mjini Singida imeahidi kutumia fursa hiyo ya udhamini wa SportPesa
vizuri kwa kuimarisha kikosi kila idara na kujitahidi kuchukua
ubingwa msimu ujao ili waweze kushiriki Michuano ya kimataifa.
Kampuni ya SportPesa wameendelea
kutumia nafasi ya makabidhiano na makubaliano hayo ya Mkataba wa
udhamini kwa kuonesha mashabiki na wapenda michezo Jezi
zitakazotumiwa na Singida United msimu ujao wa ligi kuu Tanzania
bara.
No comments:
Post a Comment