“Nchi hii kama itaamua kuwekeza kwenye uvuvi itaweza kukuza GDP,kwa kiwango ambacho
hatutaweza kuamini lakini hata sisi wabunge tutakubaliana na wazo hili kwa
kuingia kwenye"Blue economy.”
Amempongeza mh Rais na serikali ya awamu ya tano kwa
kuendelea kufanya mambo makubwa kwenye maeneo mbalimbali,kama kuanza kwa ujenzi
kama njia za juu(fly over) zinazoendelea kujengwa dar es salaam,ndege zimenunuliwa na zinaendelea
kuletwa,barabara zinaboreshwa kila kukicha.
Alimalizia kwa kusisitiza juu ya kuishauri serikali kwa
ujumbe huu “Amwambia Waziri na serikali kuwa inatakiwa iweze kununua meli
yake ya uvuvi ambayo ni ya kisasa ili
kuweza kukamilisha kazi hiyo kwa kiwango,kinachotakikana”
No comments:
Post a Comment