Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli leo Mei mosi, 2017 amehutubia kwenye
maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani iliyofanyika kitaifa
katika Viwanja vya Ushirika Moshi, mjini huko mkoani Kilimanjaro
Rais Magufuli ameeleza ni muhimu
tukaendelea kujenga uchumi wa Tanzania mpya,ameahidi serilkali
kuongeza onezeko la kawaida la mshahara na huku promosheni
zikizingatiwa kwakuwa zoezi la kusafisha nyumba iliyokuwa imejaa
uchafu limekamilika
Pamekuwa na matatizo mengi sana ya
udanganyifu mwingi,amesisitiza kuwa patakuwepo na kulipwa kwa malimbikizo,sambamba
na ongezeko la mshahara lakini pia ameahidi kutoa ajira takribani
52,000 kikubwa wafanyakazi wote kwa ujumla tunapaswa kulinda
amani,kupambana na janga la madawa ili kuwa na taifa lenye vijana
wanaojitambua na kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia vipaumbele vya serikali kuelekea kwenye uchumi wa viwanda.
Na hii ni kauli mbiu aliyoitoa:>>>"uchumi wa viwanda uzingatie kulinda haki,maslahi na heshima ya wafanyakazi"
No comments:
Post a Comment