Baada
mafuriko yamashabiki wa muziki nchini Zambia kukata kiu zao za
burudani,kwa shoo kali toka kwa Diamondplatnumz,ndipo Chibu ameona aje
na shauri huu kwa wasanii wote Tanzania,ameandika haya kupitia
ukurasa wake wa instagram..
"Leo
ningependa nitoe ujumbe huu kwa wasanii wenzangu pendwa... Siku hizi
mjini kila mtu anajifanya yeye soko la Muziki analijua sana na bingwa
wa kuelekeza na kukosoa nyimbo za watu....pasipo kujua kuwa kila
nyimbo ina soko lake na kila mwanamziki anapotoa nyimbo anakuwa na
malengo ama plan ambayo kaidhamilia...leo ntakupostia baadhi ya
nyimbo ambazo wakati nazitoa zilidharauliwa, zilipingwa sana na
wanaojifanya wajuaji wa Muziki... pasipo kujua kuwa dhamira ama nini
yalikuwa malengo yangu....kwakuwa nilikuwa na imani na kufahamu
nikifanyacho basi nikawa nawaekea tu neno #MALENGO na leo hii nyimbo
hizo ndio sababu kubwa ya mimi kuwa na Show za nchi ambazo kiukweli
sijawai tegemea fika na kufanya show za Uwanjani..... sababu yangu
kubwa leo ni kuwasihi wasanii wenzangu kuwa mnapokuwa na kitu ambacho
mnamalengo ama target nacho msiogope kukisimamia...lakini pia
kuwajuza kuwa kila kanda ina maadhi ya muziki wake ambao unaupenda,
hivyo ukitaka kufanikiwa kushika kanda zote usiogope kufanya Muziki
tofautitofauti ili kuongeza Mashabiki ila ukiogopa kufanya muziki wa
mahadhi flani kisa wabongo wataongea na kuamua tu kutoa kina
"UKIMUONA" Basi hatutafanikiwa kuteka Masoko na chi
zingine...#SimbaInZambia
"
No comments:
Post a Comment