Siku
ya mei mosi ambayo ni siku ya wafanyakazi duniani ilikuwa na
changamoto katika nchi ya Venezuela ambapo zilizuka vurugu na
maandamano miongoni mwa wananchi kumpinga rais wa Venezuela Nicolas
Maduro kwa kile alichoeleza kwenye hotuba yake.
Rais Maduro,
alipendekeza liundwe Bunge la katiba ambalo litakuwa na mamlaka ya
kuandika katiba mpya,kwa madai kuwa chombo hicho kipya kitaundwa na
raia wa kawaida,na kuachana na bunge la kitaifa linaloonekana kuwa na
wapinzani wengi.
Kwa
upande wa kiongozi wa Upinzani, nchini Venezuela, Henrique Capriles
amesema chombo hicho kipya kitakuwa kina malengo ya kuhujumu katiba
.Na mara kdhaa imeonekana Bunge la kitaifa likitaka Rais Maduro
ajiuzulu kutokana na taifa hilo kuendelea kukabiliwa na hali mbaya
na isiyoridhisha kiuchumi
No comments:
Post a Comment