• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Tuesday, 30 May 2017

    Klabu ya Huddersfield Town imefanikiwa kupanda daraja kwa kuingia rasmi Epl.

    Klabu ya Huddersfield Town imepandishwa daraja kucheza Ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya kwanza baada ya kuichapa Reading 4-3 kupitia mikwaju ya penalti uwanjani Wembley Jumatatu.
    Baada ya kutoka sare 0-0 dakika 120, Town walitakiwa kupiga penalti na wakawa na bahati ambayo kwao imejirudia kwa mara nyingine kwani kwenye nusu fainali waliwachapa Sheffield Wednesday kwa mikwaju ya penalti pia.
    Christopher Schindler aliwafungia Huddersfield Town baada ya penalti ya Liam Moore kupaa angani nao mpira wa Jordan Obita ukaokolewa na kipa Danny Ward.Klabu hiyo ya Yorkshire Magharibi haijacheza soka ya ligi kuu tangu 1972.


    Reading, waliomaliza alama nne na nafasi mbili juu ya Town waliokuwa nafasi ya tano katika ligi ya Championship sasa wameshindwa katika fainali ya muondoano ya kufuzu kwa EPL baada ya ligi kwa mara ya nne.

    No comments:

    Post a Comment