• DON'T MISS

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****

    *****ADVERTISE HERE WITH US*****
    RABA CLASSIC

    Tuesday, 30 May 2017

    Arsene Wenger amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka miwili,kubaki The Gunners.

    Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amekubali kuchukua mkataba wa miaka miwili katika klabu hiyo, jambo ambalo litamfanya kocha huyo kusalia The Gunners hadi mwishoni mwa mwaka 2019.



    Wenger na mmiliki wa klabu hiyo Stan Kroenke, walikutana hapo jana kuamua mustakabali wa meneja huyo, na kisha uamuzi wao ukawasilishwa katika mkutano wa bodi hii leo.Maamuzi yaliyo fikiwa katika kikao hicho cha bodi ya Arsenal yata tangazwa rasmi siku ya Jumatano hii, mkataba wa Wenger ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu.


    Hivi karibuni baadhi ya mashabiki wa Arsenal wamekuwa wakimtaka Wenger ajiuzulu, hasa baada ya matokeo mabaya msimu huu. Shutuma zaidi zilitolewa baada ya kufungwa jumla ya mabao 10-2 na klabu ya Bayern Munich katika hatua ya 16 bora ya klabu bingwa barani ulaya.

    No comments:

    Post a Comment