Diamond Platnumaz weekend hii alishambuliwa na mashabiki
wake katika mitandao ya kijamii kutokana na kitendo chake cha kufanya show
nchini Kenya licha ya mama watoto wake, Zari kufiwa na mume wake huyo wa
zamani.
Meneja wa msanii huyo, Sallam amesema kuwa Diamond ameshindwa kuhudhuria mazishi hayo
kutokana na ratiba kuingiliana.
“Kwenye mazishi hatujahudhuria, ilikuwa twende leo alfajiri
lakini sasa kumbe wao wametoka usiku kwenda kijijini. Kwa hiyo nadhani ratiba
yetu imeingiliana maana na sisi tulitoka Nairobi jana jioni.” Sallam alikiambia
kipindi cha U-heard cha Clouds FM.
Aidha Sallam amekanusha taarifa za kwenye mitandao ya
kijamii kwamba wameshindwa kuhudhuria mazishi hayo baada ya kuzuiwa airport
kuingia nchini Uganga kutoka na ishu za usalama.Ameeleza kuwa wao walitaka kuhudhuria mazishi hayo kwaajili
ya kumpa pole Zari na wana familia wote.
No comments:
Post a Comment