Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison
Mwakyembe amesema Tanzania inarekodi nzuri katika kuheshimu na
kulinda uhuru vya habari miongoni mwa nchi za Afrika.
Aidha katika kujibu maswali ya Wabunge waliochangia Bajeti ya
Wizara ya Habari kwa Mwaka wa fedha 2017/2018, Dkt Mwakyembe amesema
hata utafiti uliofanywa kila mwaka na shirika la Waandishi wa Habari
wasio na mipaka inaonyesha Tanzania imekuwa ikilinda uhuru huo wa
vyombo vya habari. Imeweza kushika nafasi ya 83 katika takwimu
iliyofanywa na shirika hilo la wanahabari wasio na mipaka.
“Mimi ninachosema na naomba waheshimiwa wabunge mnielewe nasema
laiti hawa reporters without borders wangekuwa wanafanya utafiti wao
Kisayansi mimi naamini Tanzania tungekuwa tumeshika nafasi bora
zaidi.”
Dkt Mwakyembe ameeleza kuwa kauli zinazotolewa na baadhi ya watu
kuwa Tanzania kuna ukandamizaji wa uhuru Vyombo vya Habari,si za
kweli huku akisisitiza kwa kusema kuwa serikali imekuwa ikihamasisha
uundwaji vyombo hivyo katika uwazi.
No comments:
Post a Comment