Klabu ya Everton ya nchini Uingereza inatarajia kuzulu nchini
Tanzania kwa mchezo wa kirafiki kabla ya msimu wa 2017/18. Ziara hiyo
inakuja baada ya klabu hiyo kuwa chini ya udhamini mpya wa
Sportpesa.
Klabu hiyo itashuka dimbani dhidi ya Timu na wachezaji wa ligi kuu
Tanzania,waliopo chini ya udhamini wa sportpesa na mshindi wa kombe
la wadhamini hao,huu mchezo utachezwa pale uwanja Taifa wa Dar es
salaam Julai 13.
Everton inatarajiwa kuwa klabu ya kwanza ya ligi kuu Uingereza
kuja kucheza nchini Tanzania,kampuni ya sportpesa imeendelea
kujitanua kwa kuwekeza na kuvidhamini vilabu katika ligi tofauti
duniani.
No comments:
Post a Comment