WCB CEO “Diamond
Platnumz” kupitia Clouds 360 ya Clouds
TV amemtambulisha msanii mpya ambaye atakuwa miongoni mwa wa wasanii wa kundi hilo,Diamond amesema kuwa
anawajibika kuwasaidia wengine kwa kuwa nae amesaidiwa mpaka hapo alipofikia hivyo anapenda na wengine wakifikia mafanikio
kama yake na hata kumzidi kwa kusaidiana
nao”.
“Ujio wangu
hapa leo ni kwa ajili ya kumtambulisha kijana wetu mwingine kama sehemu ya
kuwasaidia wengine,kijana anatambulika kama "LavaLava" ambaye anakuja na ujio wa wimbo unaoitwa "bora tuachane"ambapo unapatikana ndani ya "wasafi.com". Nawashukuru sana Clouds Media kuwa kama daraja kuwasaidia
wengine. Kama nisingesaidiwa nisingefika hapa. Inapotokea mtu anasaidiwa
nashiriki kwa kidogo nilichonacho kwa sababu mimi nisingesaidiwa nisingefika
hapa”.
“Nimekuwa mtu
wakupenda kuwasaidia wengine kwenye mambo tofauti kwani name nimesaidiwa
sana,kwenye mambo yangu,na mpaka sasa nitaendelea kupewa msaada kwa mambo
yatakayohitaji ka kufanya hivyo”
“Moto wa Clouds ni Redio Ya Watu, na Televisheni Ya Watu kwa hiyo nawashukuru kwa sababu hawaishii kwenye burudani tu wanakuwa karibu na watu kwa kuishi kwenye maisha yao halisi. Nafahamu mangapi Clouds wamenisaidia na siwezi kusahau.” -Diamond Platnumz.
No comments:
Post a Comment