Klabu ya
Chelsea wakiwa ugenini wamechukua ubingwa wa Ligi Kuu ya England
(EPL)baada ya kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya West Bromwich. Goli hilo la
ushindi Chelsea lilifungwa na Michy Batshuayi katika dakika ya 82.
hii imekuja baada ya kushinda pia
kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Middlesbrough walipopata ushindi
mnono wa goli 3-0 siku ya tar 08/05/2017, na walikuwa wakiusubiri
mchezo wao dhidi ya west brom kwa hamu na matamanio makubwa ya
kuukimbilia ubingwa huo wa ligi kuu ya Uingereza. Timu ya chelsea
imechukua ubingwa huo wa Uingereza ikiwa na michezo miwili mkononi.
No comments:
Post a Comment