Ile siku ambayo ilikuwa inasubiriwa na wengi hasa wapenzi wa
mchezo wa ngumi duniani, imewadia ambapo tambo na majigambo ya
kutunishiana misuli yatafika mwisho punde mpambano huu
utakapomalizika.
siku hii Jumamosi ya tarehe29 April, 2017 kwenye uwanja wa Wembley
jijini London ambapo litashuhudiwa lile pambano kali la mchezo wa
ndondi litakalowakutanisha miamba wawili kutoka Uingereza na Ukraine,
Anthony Joshua naWladimir Klitschko.
Aidha pambano hilo limetanguliwa na tambo nyingi kutoka kwa
mabondia hao ambao kila mmoja ametamba kuibuka bingwa dhidi ya
mwenzake. Na mashabiki wanaokadiriwa kufikia 90,000 watatarajiwa
kuingia katika uwanja wa Wembley mjini London.
Ninakuletea picha yenye rekodi inayowachambua wakali hawa:
No comments:
Post a Comment