Siku chache zilizopita zilizuka tetesi kwamba mastaa
wawili wa muziki ambao wako katika mahusiano ya kimapenzi, Vanessa
Mdee na Jux wameachana.Tetesi ambazo zilizua gumzo katika mitandao ya
kijamii, ikiwa hatukupata kauli yoyote kutoka kwa wahusika hao
wawili.
Kwenye kipindi cha XXL ya Clouds FM Jux alikuwa
akitambulisha ngoma yake mpya ambayo inakwenda kwa jina la "Umenikamata", lakini moja kati ya maswali ambayo aliulizwa ni kuhusu
tetesi za kuvunjika kwa mahusiano yake na Vanessa.
Aidha JUX amekanusha tetesi hizo kwa amedai kwa
amesema kuwa wanaosambaza uzushi kuwa ameachana na vanessa mdee kuwa
sio kweli,kwani wako vizuri sana,anasema anaelewa wao wako kikazi
zaidi na anapenda watu pia waelewe hivyo.
Aliongeza kwa kusema watu wote tunapaswa kuwasapoti
wanawake wanaofanya muziki ili kuwatia moyo kwa kile wanachokifanya
na sio kuwakatisha moyo tu.
No comments:
Post a Comment