Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon
Sirro
amesema
kuwa Jeshi hilo limewakamata watu saba katika tukio hilo na tayari
Jalada limepelekwa kwa Wakili wa serikali kwa ajili ya kulisoma na
kuandaa mashtaka ili wafikishwe Mahakamani.
Amewaomba
wote waliojijua kuwa wamehusika na kufanya,fujokwenye tukio la
mkutano wa CUF,wajitokeze lakini amebainisha watu saba wameshakamatwa
na taratibu zinaendelea kwa sasa,na jalada limefunguliwa na kupelekwa
kwa mwana sheria ili sheria ifuate mkondo wake.
Ametoa
katazo kwa maandamano yasiyo ya msingi,na kama kuna makatazo ambayo
yamewekewa,mipaka inatakiwa tuzingatia.
Alimalizia
kuwa oparesheni mbalimbali zinaendelea vizuri,dawa ya kulevya
yanaendelea kukamatwa kwa waliojihusisha,kwani wamekamata wezi wa
pikipiki na wameendelea kutoa ushirikiano kwa kusaidia kupatikana
mtandao wao,lakini pia wameshakamata magari kadhaa pamoja na mmoja wa
wamiliki wa gereji bubu ambayo imekuwa ikipokea magari yanayoibiwa.
No comments:
Post a Comment