Kiungo wa timu ya soka ya Simba ya Dar
es salaam ,”Mzamiru Yassin” ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa
mwezi march 2017 ya timu ya Simba,ambapo Mwezi wa tatu Simba ilicheza
michezo mitano ambayo ni mchezo dhidi ya Mbeya
City kwenye ligi kuu, wakacheza na Madini
Fc kwenye kombe la shirikisho. na mechi tatu za kirafiki dhidi
ya “Polisi Dodoma, Chemba Kombaini, na
Mererani Kombaini”
Simba imekuwa na utaratibu wa kumchagua mchezaji yoyote ambae ameonyesha kiwango skizuri na kuisaidia timu kupata matokeo mazuri kwenye michezo yake na kumtunuku tuzo hiyo kama motisha na hamasa kwa wachezaji wake ili waweze kuwa na morali ya kujituma na kuonesha uwezo mzuri utakaokuwa na tija kwenye timu.
Wachezaji wengine ambao wameshawahi kunyakua tuzo hiyo ni Abdi Banda ambaye alipata mwezi Februari, Laudit Mavugo mwezi wa Kwanza. Hii ni Mara ya pili kwa Mzamiru Yassin kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwezi kwa timu ya Simba.
No comments:
Post a Comment