Iile sakata la kuzuiwa kwa
uuzwaji na usambazaji wa movie za nje ambazo zimetafsiriwa kwa lugha
ya kiswahili,ambazo zimeonekana kuliangusha soko la filamu za kibongo
limeendelea kushika chati kwani watu mashuhuri wameendelea kutoa
ushauri na mitazamo yao juu ya jambo hilo.
Mkali wa Hiphop Tanzania “Fareed
Kubanda maarufu kama Fid Q” ametoa ushauri wake kupitia
kipindi cha “leo Tena cha Clouds FM “ kilichorushwa siku ya tarehe 28 april 2017.
Fid Q amesema “harakati
ambazo zinafanywa na mastaa wa Bongo Movie ni nzuri na wanahitaji
kusapotiwa juu ya hili ili malengo yafikiwe”.
Fid Q amewashauri wasanii na wadau wa Bongo Movie
kuwa kitu kimoja, na kufanya kazi kama team na kutoa kazi zao kwa
mpangilio ili kuzifanya kazi hizo kufika mbali tofauti na kuwa kwa
wiki wanatoa filamu 5 au 10 ambazo zitakosa mpangilio mzuri
utakaopelekea kuzorota kwa tasnia hiyo.lakini amesisitiza wajaribu kukaa chini na serikali ili wapate sapoti na kuongeza uhalisia katika kazi zao
No comments:
Post a Comment