Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewasili
mkoani Kilimanjaro kwa ziara ya siku tatu, ambapo anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi katika sherehe ya wafanyakazi ‘Mei Mosi’.
Mh
rais amewashukuru wananchi wa mkoa wa kilimanjaro kwa kujitokeza kwa
wingi na kuonesha kuiamini serikali yake,amesisitiza mshikamano baina
ya watanzania wote ili kuweza kusukuma gurudumu la maendeleo ya
tanzania.
Ameeleza
kwa msisitizo kuwa maendeleo hayana vyama,”hakuna
mtanzania anayekula vyama,na sababu ya kuja hapa ni kuweza kuungana
na wananchi wa kilimanjaro na taifa katika kuibua na kuondoa
changamoto zinazowakabili wanachi wa Tanzania kwa ujumla”asanteni
sana,sana alimalizia mh Rais JPM.
No comments:
Post a Comment