Nusu fainali ya kwanza ya
Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC)msimu wa 2016/17 ilichezwa
uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo walikutana timu za Simba dhidi
ya Azam FC.
Simba imefanikiwa kupata
ushindi huo wa kwanza dhidi ya Azam FC kwa mwaka 2017 baada ya kupoteza
michezo yao miwili kati ya mitatu waliyocheza dhidi ya Azam FC kwa
mwaka 2017, na wamefanikiwa kuupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Mohamed
Ibrahim.
Simba sasa inasubiri
mshindi wa mchezo wa nusu fainali kati ya Yanga dhidi ya Mbao FC
mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza siku ya april
30,2017.
No comments:
Post a Comment