Kwenye
pambano la masumbwi la usiku wa April 19 mashabiki wa mchezo huo
walishuhudia mpigano wa kihistoria,ambapo Anthony Joshua alimwangusha
Wladimir katika raundi ya tano,lakini mambo yalimgeukia kwenye raundi
ya 6 ambapo nae aliangushwa kwa mara ya kwanza tangu alipoanza mchezo
huo.
Joshua
alitumia vizuri nafasi kidogo aliyoipata katika hatua ya kuufikia
ushindi,kwa kutupa ngumi za kushtukiza zilizompeleka chini mpinzani
wake na raundi ya 11 ndipo pambano liliposimamishwa.
Uwanja wa Wembley ulitawaliwa na shangwe pindi mwamuzi aliposema kuwa Wladimir Klitschko amezidiwa na hatoendelea na pambano,Hivyo AnthonyJoshua ambaye pamoja na umri wake wa miaka 27 na kushinda mechi zote 18 za awali alizocheza kwa ushindi wa KO,hivyo pambano la jana litajumuisha michezo 19 aliyoshinda na kuzidi kujiwekea rekodi ya ubora katika katika tasnia hiyo ya ndondi za uzani wa juu.
No comments:
Post a Comment