Wakala
wa Usajili, Ufilisi na Udhamini nchini (RITA), umempa Tuzo, aliyekuwa
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt Harrison Mwakyembe, kwa kutambua
mchango wake katika kuboresha hali ya usajili wa matukio muhimu ya
binadamu nchini
Dkt
Mwakyembe amekabidhiwa Tuzo hiyo na Waziri wa Katiba na Sheria,
Profesa Palamagamba Kabudi, katika Ofisi za Wizara mjini Dodoma.
Kwa
upande wa Profesa Kabudi, amempongeza Dkt Mwakyembe kwa jinsi
alivyojitoa na kuhakikisha hali ya usajili inaboreshwa na hivyo
kuinua muamko wa wananchi na kuona umuhimu wa kujisajili na kuwa na
cheti cha kuzaliwa.
Dkt.
Mwakyembe baada ya kupokea Tuzo hiyo alisema “Sina
neno kubwa la kuwaambia zaidi ya Kushukuru kwa kusema asante”.
“Asanteni sana, niwaahidi kwamba nitaendelea kuwaunga mkono huko
nilipokwenda. Nanyi lazima muendeleze kazi ya kuhamasisha usajili kwa
nguvu zenu zote, na mjue kwamba mna kazi kubwa mbele yenu na ni
lazima ifanikiwe.”
No comments:
Post a Comment