Mbunge
wa Bariadi Andrew Chenge amesema atalazimika kuiambia serikali iache
maneno baaya ya kuwa imepita muda mrefu hadi sasa ikiahidi kufanya
ujenzi wa barabara katika jimbo lake huku utekelezaji ukichukua muda
mrefu.
Aidha
amesema anaipongeza serikali ya awamu ya tano,ambayo imeendelea
kuunganisha nchi yetu kwa miradi ya barabara nyingi na zinazopitika
ambazo baadhi zimekamilika na nyingine,zinaendelea kukamilika.
Aliendelea kuiomba serikali
kuunganisha barabara itakayo unganisha singida na simiyu kupitia
iguguno,na wilaya ya mkalama singida,mpaka kuifikia bariadi,na
kuangalia pia barabara ambayo itaunganisha simiyu na arusha.
Chenge
alimalizia kwa kusema
“Kwa
mwaka huu nakubaliana na serikali kuhusu madai yao kwamba
wamekamilisha upembuzi kuhusu ujenzi wa barabara jimboni kwangu,
mwaka kesho kama ikiendelea hivi mimi nitasema waache maneno waweke
muziki
“
No comments:
Post a Comment