Waziri
Kairuki amebainisha hayo leo katika ukumbi wa Chimwaga uliopo ndani
ya Chuo Kikuu cha Dodoma, wakati anatoa taarifa ya uwasilishaji wa
uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa umma,lilioendeshwa na Serikali
kuanzia mwezi Oktoba mwaka 2016.
“Zoezi
hili la uhakiki wa vyeti feki kwa watumishi wa umma liliwahusisha
watumishi wa umma pekee wakiwemo makatibu wakuu,watendaji na maofisha
wengine mbalimbali wa ngazi za serikali, zoezi hili halikuwahusisha
viongozi wa kisiasa” alisisitiza waziri Kairuki.
“Watumishi
9,932 wamebainika kuwa na vyeti vya kughushi sawa na asilimia 2.4,
Wenye vyeti vyenye utata ni 1,538 vilikuwa vikitumiwa na jumla ya
watu 3,076, wenye vyeti halali pekee ni asilimia 94.23. Hatua
zitachukuliwa kwa wenye vyeti feki pamoja na,bali hata kwa wahusika
waliotengeneza vyeti hivyo”.
Waziri
Kairuki alimaliza kwa kusema wale wote wanajijua wanatumia vyeti vya
kughushi waache mara moja, kwa kuwa ni kosa la jinai huku akisisitiza
kuwa adhabu yake ni kufungwa jela miaka saba.
No comments:
Post a Comment