Waziri mwenye dhamana ya michezo Dr. Harrison Mwakyembe azungumza baada ya taarifa ya kwamba timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ ilishushwa kwenye mabasi na TRA wakati ipo njiani kwenda kwa makamu wa Rais mama Samia Suluhu Hassani ambaye aliialika timu hiyo nyumbani kwake.
Mwakyembe
amesema ni aibu kwetu kama taifa hasa kwa kipindi hiki ambacho
watanzania tunapaswa kuunganisha nguvu zetu katika kuhamasisha
michezo na kuwatia moyo wachezaji wetu ili timu ifanye vizuri na sio
kukwamisha jitihada za kuinua michezo kote nchini.
“Vijana
wetu walikuwa wanakwenda kwa kiongozi wetu kwa mwaliko, lakini basi
lao likasimamishwa na watu wa TRA kisha wakaondolewa kwenye mabasi na
magari kuchukuliwa, ikabidi viongozi wa TFF waanze kutafuta magari
mengine, ili kukamilisha safari hiyo”
Aidha waziri Mwakyembe amewaomba TRA kuendelea
kufanya kazi yao kwa mujibu lakini pia kutumia busara pale inapobidi.
Baada
ya tukio hilo,Waziri mwakyembe amemwagiza katibu mkuu wake kukaa na
katibu mkuu wa Wizara ya Fedha na viongozi wa TRA kwa pamoja,ili
kuepusha aibu za namna hii kwa wakati mwingine.
“Nasema
kwa masikitiko kwa sababu timu hii ilipoanza nilikuwa nawafuatilia
sana, mechi yao ya kwanza ilibidi wasafiri hadi Kigoma kwa basi kwa
sababu akaunti za TFF zilifungwa, wakafika Kigoma wakiwa hoi kwa
safari ndefu ikabidi waiombe timu ya Burundi kuja Kigoma kucheza nao,
wakafungwa 2-1. Sasa leo basi lao linakamatwa wakati tupo kwenye
kampeni ya kitaifa kuhakikisha vijana wanafanya vizuri na kuliletea
sifa taifa”.
Baadae
usiku, ilitoka taarifa kutoka kwa afisa habari wa TFF Alfred Lucas
kwamba, kampuni ya udalali ya Yono ambayo ni wakala wa TRA imetangaza
kuliachia mara moja basi ambalo linatumiwa na Serengeti Boys.
No comments:
Post a Comment