Chombo cha dola kimendelea kutoa ufafanuzi,juu ya taarifa za tukio la
kupotea kwa Msanii wa Bongo Fleva hapa nchini, “Ibrahim Mussa”
maarufu kwa jina la “Roma Mkatoliki” na wenzake,pia kuendelea kuwaomba
wasanii na wananchi kwa ujumla kuendelea kuwa watulivu katika kipindi
hiki.
Aidha kimendelea kusema kwa yeyote atakayepata taarifa zitakazosaidia katika
upelelezi wa tukio hili atoe ushirikiano kwenye vyombo vya dola
mapema.
Haya
yamesemwa na kamanda wa polisi kanda maalumu Dar es salaam Simon
Sirro,na hii ni baada ya kutokea kwa tukio hilo mapema hii,hivyo basi
amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi limeendelea na hatua za kipelelezi
wa tukio hilo mapema baada ya taarifa kuwafikia.
Ameongeza
kwa kuwaomba baadhi ya watu kutokuwa wepesi wa kusambaza uvumi
pasipokujua uhalisia au undani wa jambo kabla hawajaliongelea.
“unajua
mambo ya uvumi sio mazuri,kikubwa tuviachie vyombo husika vifanye
kazi yake na kuvisaidia pale inapobidi” alisisitiza kamanda Sirro.
No comments:
Post a Comment