Waandamanaji walikusanyika katika miji mbalimbali nchini humo wakimtaka rais huyo kujiuzulu baada ya kufutwa kazi kwa waziri wa fedha,vikundi vya watu waandamanaji vimeonekana katika miji ya Johannesburg, Cape Town, Durban na mji kuu wa Pretoria.
Hatua
ya Zuma kumtoa Pravin Gordhan kwenye nafasi yake kama waziri wa
fedha ilipokelewa kwa hisia tofauti na kupelekea maandamano hayo,ambapo masoko ya hisa yalishuka pia.
Maelfu
ya watu walitarajiwa kuandamana ,baada ya picha za matukio ya waandamanaji
kuendelea kusambazwa katika mitandao ya kijamii zikionyesha vikundi
vikubwa vya watu katika maeneo tofauti ya majiji nchini humo.
No comments:
Post a Comment