TANZANIA imepanda Kwa nafasi 22 kwenye viwango vya FIFA duniani kutoka nafasi ya 157 na kwa sasa imeshika namba135. Hii imetokana na Tifa Stars kutembeza kichapo kwenye mechi mbili mfululizo za kirafiki dhidi ya Botswana waliyoshida kwa magoli 2-0 na Burundi iliyoshinda kwa magoli 2-1.
Brazil
imekamata namba moja,ikifuatiwa na Argentina,ambayo ilikuwa kwenye nafasi ya kwanza
kwa miezi kadhaa ikishikilia usukani huo.
Haya
ndio mataifa kumi yanayoongoza kwenye viwango vya soka Duniani.
1.
Brazil 2. Argentina 3. Germany 4. Chile 5. Colombia 6. Ufaransa 7.
Ubeligiji 8. Ureno 9. Uswisi na 10. Hispania.
Mataifa
10 yanayongoza Afrika na nafasi zao za viwango vya ubora duniani.
1.
Misri (19) 2. Senegal (30) 3.C ameroon (33) 4. Burkinafaso (35) 5.
Nigeria (40) 6. DR Congo (41) 7. Tunisia (42) 8. Ghana (45) 9. Ivory
Coast (48) 10. Morocco (53)
Kwa
Afrika Mashariki Uganda inaendelea kuongoza ikiwa nafasi 72 ikiwa
imepanda nafasi 3 kutoka 75 ya mwezi wa Pili, Kenya nafasi 78 nayo
ikiwa imepanda Kwa nafasi 10 kutoka 88 ya Mwezi uliopita wakati
Rwanda yenyewe inakamata nafasi ya 117 ikiwa imeshuka kwa nafasi 17
kutoka nafasi ya 100 ya mwezi uliopita na Burundi ambao ilifungwa na
Tanzania ipo katika nafasi ya 141 nayo ikiwa imeshuka kwa nafasi 3
kutoka nafasi ya 138 ya mwezi wa pili.
No comments:
Post a Comment