Uongozi wa Simba Sc umewasilisha rufaa Kwenye Bodi ya ligi shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kudai pointi za mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Jumapili ya wiki iliyopita uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba na Simba kufungwa kwa magoli mawili kwa moja (2-1) na Kagera Sugar.
Kwenye barua ya Simba imedai Kagera Sugar ilimtumia mchezaji Mohamed Fakhi mwenye kadi tatu za njano ambapo ni kinyume na kanuni na taratibu za ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara .
Kamati ya masaa 72 inatarajiwa kupitia rufaa mbalimbali zilizowasilishwa kwenye kamati na hatimae kuja na maamuzi
Wakati haya yakiendelea uongozi wa Kagera Sugar umejitokeza na kusema,
"Mimi ni mtu makini sana kwenye jambo linalomgusa mchezaji wangu, kila mchezaji wangu anapoonyeshwa kadi huwa natunza kumbukumbu na pia namkumbusha meneja wangu kuandika pi,Simba kama wameshindwa kutafuta pointi uwanjani wasitafute sababu ya kupata pointi za mezani".
Meneja wa kikosi cha kagera sugar amesema Fakhi ana kadi mbili tu za njano na si tatu Kama ilivyovyosema.
No comments:
Post a Comment