Zaidi
ya watu 90 wanahofiwa kufa maji huko pwani ya libya,ambapo
inasemekana mashua ambayo inakadidriwa kubeba wahamiaji 120
ilizama,shughuli za uokoaji bado zinaendelea.
Njia
hizo za baharini zimekuwa zikitumiwa na wahamiaji na wakimbizi wengi
kuingia kusini mwa Ulaya kutafuta hifadhi, Aidha msemaji wa kikosi
cha ulinzi pwani ya mji wa Tripoli “Ayoub Kassem”, amesema
anaamini kuwa kila mtu ambaye alikuwa katika mashua hiyo alitoka nchi
za kusini mwa jangwa la sahara.
Watu
23 kati ya watu 120 waliokolewa baharini,na wamepelekwa kwenye
hifadhi na uangalizi na walieleza kuwa kati ya waliozama kuna kundi
la watoto na wanawake.
No comments:
Post a Comment